Baraka FM

Chunya yapiga hatua kimaendeleo

26 August 2024, 15:32

Jengo la utawala halmashauri ya wilaya ya Chunya Mbeya

Chunya ni moja ya halmashauri inayounda mkoa wa Mbeya ambapo kwa sasa halmashauri hiyo imefunguka kiuchumi tofauti na miaka ya nyuma, kwasasa halmashauri hiyo inafikika kirahisi kutokana na uwepo wa barabara nzuri huku ikisifika katika uchimbaji wa madini pamoja na kilimo Cha Tumbaku.

Na Hobokela Lwinga

Serikali kupitia halmashauri ya wilaya ya chunya imeendelea kukamilisha miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo kukamilisha jengo la utawala, ujenzi ofisi za madini pamoja na uwanja wa michezo ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za karibu kwa wananchi.

Hayo yamebainika katika ziara maalumu iliyofanywa na mchekeshaji nguli nchini na Askofu wa makanisa yaFeel Free church mchungaji Emanuel mgaya maarufu kwa jina la Masanja mkandamizaji alipotembelea miradi na kujionea namna ambavyo inatekelezwa.

Masanja amesema ili wananchi waendelee kunufaika kupitia serikali yao hawana budi kuiunga mkono kwa kutoa ushirikiano kwa viongozi wanaowaongoza.

Mchekeshaji nguli nchini na Askofu wa makanisa ya Feel Free church mchungaji Emanuel mgaya(picha na Hobokela Lwinga)
Sauti ya mchekeshaji nguli nchini na Askofu wa makanisa yaFeel Free church mchungaji Emanuel mgaya

Akitoa taarifa ya ujenzi wa uwanja wa michezo unaojengwa katika halmashauri ya hiyo, mwenyekiti wa kamati ya ujenzi Ayoub Omary amesema uwanja huo utajengwa ili kukidhi vigezo vya kimataifa ambavyo vitawezesha kufanyika katika michezo ya ndani na ya kimataiafa huku akisema uwanja huo utaongeza soko la ajira kwa vijana.

Sauti ya Mwenyekiti wa kamati ya ujenzi Ayoub Omary

Kwa upande wake afisa madini wa wilaya ya chunya Maulid Kimweli amesema serikali imeendelea kuboresha mazingira mazuri kwa wachimbaji na wanunuzi kwa kujenga soko la madini ambalo litasaidia kupata huduma kwa ukaribu.

Sauti ya afisa madini wa wilaya ya chunya Maulid Kimweli

Halmashauri ya chunya ni moja ya halmashauri ambayo imepiga hatua kubwa ya kimaendeleo ambapo mpaka sasa imekamilisha ujenzi wa jengo la utawala, sambamba na ukamilishaji wa miradi ya miundombinu ya elimu,afya,barabara pamoja na kuboresha sekta ya kilimo.