Viongozi watakiwa kuhimiza michezo kuchochea ajira kwa vijana
30 July 2024, 18:40
Michezo ni afya na ndiyo sababu wataalam wa afya wamekuwa wakihimizwa ufanyaji wa mazoezi kwani husaidia kujiepusha na magonjwa yasiyoambukizwa.
Na Hobokela Lwinga, Mbeya
Viongozi mbalimbali wametakiwa kulipa kipaumbele suala la michezo kwenye maeneo yao hali itakayoimarisha ushirikiano katika kuchochea maendeleo ya mtu mmoja na taifa kwa ujumla.
Hayo yamesemwa na mjumbe wa kamati kuu ya Chama Cha Mapinduzi Noah Mwakisu wakati akimwakilisha mjumbe wa kamati ya CCM taifa Ndg. Ndele Mwaselela katika ufungaji wa ligi ya mpira wa miguu Mwashibanda Cup iliyofanyika kata ya Shizuvi halmashauri ya Mbeya.
Ndugu Mwakisu amesema mpira umetoa ajira nyingi kwa vijana hivyo kila mtu anapaswa kuithamini sekta hiyo ya michezo.
Kwa upande wake diwani wa kata ya Shizuvi ambaye ndiye mwandaaji wa mashindano hayo Noah Mwashibanda amesema wanathamini michezo kwenye kata yao kwani imewakutanisha watu mbalimbali huku akisema mshindi wa kwanza amepata zawadi ya ng’ombe.
Hata hivyo mratibu wa mashindano hayo Patrick Mwayinga amesema vilabu vimeonyesha uwezo mkubwa kwani time zingine zimefanya usajili wachezaji kutoka nje ya nchi.
Baadhi ya wachezaji walioshiriki ligi hiyo wamemshukru diwani wao kwa kuwaunganisha kupitia michezo kwenye kata yao.
Mashindano ya Mwashibanda cup yametamatika huku ikijumuisha timu 11 zote zikiwa ni timu zinatoka ndani ya kata ya Shizuvi.