Kwaya kuu Ushirika wa Msia Mbozi watembelea Baraka FM Mbeya
13 July 2024, 13:58
Kutembelewa ni jambo la heri na hii ni ishara kwamba unapendwa, hii ndio maana halisi ya kile kinachokuwa kimefanyika kwa mgeni yoyote anayefika katika malango yako.
Na Hobokela Lwinga
Mapema leo kituo cha matangazo cha redio Baraka kimepokea ugeni wa kwaya kuu kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Mbozi Ushirika wa Msia ambao wako jijini Mbeya kwenye ziara maalumu katika Ushirika wa mabatini kanisa la Moravian Jimbo la Kusini Magharibi.
Baada ya kufika katika taasisi hiyo wamepokelewa na mwenyeji wao Charles Amlike meneja wa kituo hicho ambapo amewatembeza na kujifunza mambo mbalimbali yanayofanywa na taasisi hiyo inayomilikiwa na kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini Magharibi.
Aidha wageni hao wameipongeza taasisi hiyo kwa urushaji wa matangazo huku wakikiri kupata usikivu Mzuri maeneo mengi ya mkoa wa Songwe ikiwemo wilaya ya Mbozi ambako unapatikana Ushirika wa Msia.
Sambamba na hayo wageni hao wameongozana na wenyeji wao kwaya kuu ya kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini Magharibi Ushirika wa Mabatini
Wageni baada ya kumaliza kutembelewa taasisi hiyo wametoa sadaka ya kusaidia uendeshaji wa kituo hicho cha redio.