Baraka FM

Fyandomo kinda fundi wa hamasa Mbeya

3 July 2024, 15:52

Sifa za mtu mwema hupaswi kumpa akiwa amelala mauti mpe akiwa hai kwani akiwa hai utakuwa umemuheshimisha.

Na mwandishi wetu

Timida Fyandomo ni Mjumbe wa Baraza Kuu la Jumuiya ya Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa kutoka Mkoa wa Mbeya.

Amechipua katika siasa za Tanzania akianzia Mkoa wa Mbeya.

Ni binti ambaye ni mbunifu na ana upendo kwa watu bila kujali rika wala hali za maisha waliyonayo.

Hivi karibuni alihamasisha mabinti wa mkoa wa Mbeya bila kujali itikadi za siasa na kuketi nao katika ukumbi wa Tughimbe ulipo jijini Mbeya kwa lengo la kuzungumza masuala yawahusuyo. Kongamano ambalo lilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa UVCCM Taifa.

Timida Fyandomo amekuwa mhamasishaji mkubwa wa mabinti kujihusisha katika masuala ya uongozi bila kusahau kueleza kwa ufasaha utendaji thabiti wa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Katika sifa zake za Upendo, amekuwa akiunga kwa vitendo juhudi za viongozi wengine katika kusaidia jamii na hivi karibuni ameonekana akijitolea vitu kadhaa ikiwemo mtungi wa gesi na godoro kwa mmoja wa wahitaji ambaye alijengewa nyumba na Mbunge wa Mbeya Mjini Dkt. Tulia Ackson.

Pamoja na hayo ya kijamii, amewezesha fulana ( T-shirt) za chama chake kwa viongozi wa UVCCM Kata zote za Majimbo ya Mkoa wa Mbeya yaani Kyela, Busokelo, Rungwe, Mbeya Vijijini, Mbeya Mjini, Mbarali na Chunya.

Ndiyo maana ninasema kuwa Mkoa wa Mbeya unayo nafasi ya kumtunza sana binti huyu ambaye ni Mjumbe wa Baraza Kuu la UVCCM Taifa Bi. Timida Fyandomo na wengine maana ni sawa na mmea uliochipua (Chipukizi) ambao unapaswa kukuzwa zaidi.