Baraka FM

Askari 49 wa zimamoto na uokoaji wavikwa nishani Mbeya

18 June 2024, 21:17

Baadhi ya Askari wa jeshi la Zimamoto na Uokoaji walio vikwa Nishani(picha na Ezra Mwilwa)

Jeshi la zimamoto kuongezewa vifaa vyautenda kazi katika bajeti ya Serikari ya awamu ya sita 2024/2025 kauli hiyo imetolewa na mkuu wa jeshi hilo Jenelali John Masunga mkoani Mbeya.

Kamishina Jenelari wa Jeshi zimamoto na uokoaji John Masunga amemuwakilisha Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kuwavika Nisha Askari wa jeshi hilo Tanzania katika viwanja vya jeshi la zimamoto na uokoaji mkoa wa Mbeya.

Kamishina Masunga amesema Askari walio vikwa nishani ni heshima ya kutambua utumishi wao katika jeshi hilo pia amewataka Askari wote kuendelea kutumikia taifa kwa moyo wote pia amesema serikali ya awamu ya sita inayo ongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inatambua utendajikazi wa jeshi la Zimamoto na Uokoaji hivyo imeahidi kuwaongezea vitendea kazi.

Jenelari kamishina wa Jeshi zimamoto Tanzania (picha na Ezra Mwilwa)

Nae mkuu wa wilaya ya Mbeya mjini Mhe Beno Malisa kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Mbeya Mhe Juma Homera amemuomba kamishina Masunga kuongeza ajira katika Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwani idadi imekuondogo sana ukilinganisha na uwingi wa matukio.

Mkuu wa wilaya ya Mbeya mjini Mhe Beno Malisa(katikati) akiwa baadhi ya viongozi wa ulinzi na usalama mkoa wa Mbeya na wilaya ya Mbeya (picha na Ezra Mwilwa)
Sauti ya mkuu wa wilaya ya Mbeya Mhe Beno Malisa

Nao baadhi ya Askari walio vikwa nishani hizo wamemshukuru Rais kwakutambua utumishi wao huku wakiahidi kulitumikia taifa na wananchi kwa ujumla.

Mmoja wa Askari akivikwa nishani( picha na Ezra Mwilwa)
Sauti za baadhi ya Askari walio vikwa Nishani hizo

Nishani zilizo vikwa ni Utumishi mrefu na Utumishi mrefu na Tabia njema kwa jumla ya watumishi 49 kutoka mikoa ya Mbeya, Songwe, Njombe,Rukwa,Katavi na Ruvuma