Baraka FM

Wazazi washauriwa kulima mazao lishe kwa watoto

5 June 2024, 18:40

Baadhi ya viongozi wa Serikali na ADP Mbozi wakitoa elimu kwa wazazi juu ya kilimo cha mazao lishe kwa watoto(picha na Lukia Chasanika)

Limeni mazao ya yenye kusaidia kujenga afya za watoto wenu katika kukuza uwezo mkubwa wa watoto.

Na Lukia Chasanika

Wazazi na walezi wameshauriwa kulima mazao lishe ili kuwasaidia watoto kupata virutubisho ambavyo vitawasaidia kukua kiakili na kimwili.

Hayo yamesemwa na afisa kilimo,Mifugo na uvuvi wilaya ya Mbeya Gidion Mapunda akiwa mgeni rasmi katika chakula cha pamoja kati ya wazazi, wanafunzi na walimu katika shule ya msingi darajani Mbeya vijinini Kilichoandaliwa kwa ufadhili wa shirika la ADP kutoka Mbozi mkoani Songwe.

Mapunda amesema mradi ambao umepelekwa na shirika la ADP katika shule mbalimbali za wilaya ya Mbeya utasaidia kupunguza udumavu kwa watoto ambao umekithiri licha ya mkoa wa mbeya kuwa na wakulima wengi.

Aidha Mapunda amelishukru shirika hilo la ADP kwa kuwa na mradi wa lishe na amewaahidi kushirikiana na shirika hilo kuhakikisha miradi yote inafanikiwa.

afisa kilimo,Mifugo na uvuvi wilaya ya Mbeya Gidion Mapunda akiendelea kutoa Elimu kwa wazazi(picha na Lukia Chasanika)
Sauti ya Afisa kilimo,Mifugo na uvuvi wilaya ya Mbeya Gidion MapundaSauti ya

Mkuu wa idara ya maendeleo ya jamii ADP Mbozi  Maneno Uledi amesema shirika hilo linajihusisha na malengo manne katika utekelezaji wake katika mikoa sita Tanzania ikiwa ni pamoja na masuala ya lishe kwa mtoto  kwa mkoa wa Songwe,Mbeya, Katavi,rukwa na Tabora.

Sauti ya Mkuu wa idara ya maendeleo ya jamii ADP Mbozi  Maneno Uledi

Kwa upande wake mwalimu mkuu wa shule ya darajani Thelesia Mbwilo amesema mradi huo wa lishe umesaidia kuwafanya watoto kubaki darasani kwa sababu wanakula shuleni chakula chenye lishe bora.

Baadhi ya wazazi wakipokea elimu ya kulima mazao lishe(picha na Lukia Chasanika)
Sauti ya mwalimu mkuu wa shule ya darajani Thelesia Mbwilo

Wakisoma risala kwa mgeni rasmi wanafunzi wamesema mradi ambao umeletwa na ADP wamefanikiwa kuwa na shamba darasa la mahindi na maharage ambapo wamevuna mahindi gunia 8 ambazo zitawasadia wazazi kupunguza kiwango cha kuchangia chakula shuleni.

Sauti za wanafunzi wakisoma risala

Wakizungumza na kituo hiki baadhi ya viongozi wa wakulima wamelishukru shirika la ADP kwa kuwapatia mradi huo ambao umeleta tija kwa watoto hivyo wanaliomba shirika kuendelea kufadhili mirdi ya lishe katika shule mbalimbali. 

Sauti za baadhi ya viongozi wa wakulima