Baraka FM

13 wafariki, 18 wajeruhiwa ajalini Mbeya

5 June 2024, 19:07

Zoezi la uokozi na uondoaji wa baadhi ya vyombo vya moto vilivyohusishwa kwenye ajali (pikipiki)-picha na Hobokela Lwinga

Huzuni imetanda jiji la Mbeya baada ya kutokea ajali ambayo imeondoa uhai wa watu.

Na Hobokela Lwinga

Watu 13 wamepoteza maisha na wengine 18 kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha magari matatu likiwamo lori, gari dogo na Coaster.

Ajali hiyo imetokea leo Jumatano Juni 5, 2024 katika mlima wa Simike eneo la Mbembela jijini Mbeya baada ya lori lililotokea Dar es Salaam kufeli breki na kugonga gari dogo na Coaster lililokuwa na abiria kutoka Tunduma mkoani Songwe.

Akizungumza eneo la tukio, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya, SACP Benjamin Kuzaga amethibitisha kutokea tukio hilo akisema wanamshikilia dereva wa lori kwa hatua zaidi.

Kamanda Kuzaga amesema majeruhi na miili ya marehemu imepelekwa katika Hospitali ya Mkoa wa Mbeya.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya,SACP Benjamin Kuzaga (Picha na Hobokela Lwinga)
Sauti ya Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya, SACP Benjamin Kuzaga

Baadhi ya mashuhuda wameomba barabara hiyo iweze kupanuliwa kwa haraka kutoka na eneo hilo kuwa hatari na kusababisha ajali za mara kwa mara.

Baadhi ya wananchi wakishuhudia ajali katika eneo la Mbembela Nzovwe jijini Mbeya(picha na Hobokela Lwinga)
Sauti za Baadhi ya mashuhuda