67% ya watoto wanatumia simu, 4% wamefanyiwa ukatili
3 May 2024, 09:43
Ukuaji wa sayansi na tenkolojia ulimwenguni umeleta changamoto ya malezi duni kwa watoto ambapo baadhi ya wazazi wamekua wakitumia mitandao ya kijamii kutoa malezi kulea watoto wao.
Na Rukia Chasanika
Katika utafiti uliofanywa juu ya matumizi ya simu kwa watoto nchini Tanzania unaonyesha asilimia 67 wanatumia simu na asilimia nne wamefanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Hayo yamesemwa na Chritabela Ngowi kutoka wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kuwa baadhi ya tafiti zinaonyesha watoto wengi wanafanyiwa ukatili kwa kutumia mitandao ya kijamii.
Ngowi amesema mitanado ya kijamii inaharibu watoto kisaikolojia na kushindwa kufanya vizuri katika masomo yao kutokana na kukaa na simu nyakati za usiku na kuangalia vitu visivyofaa katika maadili ya mtanzania.
Pia Ngowi ametumia nafasi hiyo kuwashauri wazazi kutumia muda wao kuongea na watoto na kuwaelekeza namna nzuri ya kutumia simu ili kuwalinda dhidi ya ukatili mitandaoni.
Kwa upande wake afisa mradi kutoka shirika la DSW Tanzania Shamsa Khalifan amesema kuna ukatili wa kimtandao kwa watoto hivyo shirika hilo linatekeleza mradi wa SAFA kwa kutoa elimu namna ya kutunza taarifa zao katika mindao ya kijamii.