Baraka FM

Mikutano ya idara ya uinjilisti Moravian yatajwa sababu kukua kwa kanisa

5 November 2024, 15:43

Makamu Mwenyekiti wa Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Kusini Magharibi Mch. Asulumenye Mwahalende

Kanisa la Moravian Tanzania limekuwa na utaratibu wa kuandaa Mikutano mbalimbali ya idara inayofanyika katika majimbo lengo likiwa ni kueneza injili ya kristo.

Na Deus Mellah

Uwepo wa idara za Uinjilisti katika Kanisa la Moravian Tanzania jimbo la Kusini Magharibi unatajwa kusaidia kukua kwa kanisa kutokana na kazi zake kufanyika kwa ufanisi mkubwa.

Hayo yamesemwa na Makamu Mwenyekiti wa Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Kusini Magharibi Mch. Asulumenye Mwahalende wakati akizungumza katika mkutano wa idara ya uinjilist jimbo uliofanyika ushirika wa Chimala.

Sauti ya Makamu Mwenyekiti wa Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Kusini Magharibi Mch. Asulumenye Mwahalende

Mch. Mwahalende ameziomba shirika zote ambazo hazina idara ya uinjilisti kuwa nazo kwani ni msaada mkubwa kwa kanisa.

Sauti ya Makamu Mwenyekiti wa Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Kusini Magharibi Mch. Asulumenye Mwahalende

Naye Mwenyekiti wa Kanisa la Moravian wilaya ya Mbarali Amos Mwampamba amesema mkutano huo umeleta mafanikio makubwa kwa wakazi wa kata ya chimala.

Baadhi ya viongozi kanisa la Moravian Jimbo la kusini magharibi (picha na Deus Mellah)
Sauti ya Mwenyekiti wa Kanisa la Moravian wilaya ya Mbarali Amos Mwampamba

Aidha katibu wa idara ya uinjilist jimbo Mch. Peter Mbughi amesema mafanikio ya idara hiyo ni makubwa kwa kuwa watu wengi wameendelea kuokoka baada ya kufikiwa na huduma hiyo.

Nao baadhi ya waimbaji walioshiriki katika mkutano huo wamesema mikutano hiyo imekuwa ikiwajenga kiroho na kimwili

Hawa ni baadhi ya washiriki wa Mkutano mkuu wa Jimbo kanisa la Moravian Jimbo la kusini magharibi katika ushirika wa Chimala Mbarali Mbeya (picha na Deus Mellah)
Sauti za baadhi ya waimbaji na walioshiriki wa mkutano