Askofu Pangani aonya waumini wanaofanya kampeni kwenye mikutano ya uchaguzi kanisani
28 October 2024, 16:41
Kanisa linapaswa kutokuwa na kampeni za uchaguzi wakati wa uchaguzi wa viongozi.
Na Hobokela Lwinga
Askofu wa Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Kusini Magharibi Mch.Robert Pangani ameonya watumishi wanaofanya kampeni ndani ya kanisa kuwa hatua hiyo inaweza kukwamisha kupata viongozi wazuri wa ngazi mbalimbali.
Askofu Pangani ameyasema hayo wakati akitoa salamu za Jimbo kwa waumini wa kanisa la Moravian ushirika wa Nzovwe jijini Mbeya.
Askofu Pangani amesema baadhi ya MAJIMBO katika kanisa la Moravian yameshindwa kupata maaskofu kutokana na kampeni ambazo zimekuwa zikifanywa na baadhi ya washiriki wa Mikutano ya Sinodi.
Aidha ametataja majimbo hayo kuwa ni Jimbo la ziwa Tanganyika (Kigoma) na Jimbo la kasikazini (Arusha) sambamba nakuwataka waumini kuendelea kuombea majimbo ambayo yanayotarajiwa kuwa na mikutano ya uchaguzi ikiwemo Jimbo la Mbozi.
Katika Mkutano viongozi waliochaguliwa ni mchungaji Anorld Mbulwa kuwa mwenyekiti, mchungaji Abisai Jacob kuwa makamu mwenyekiti na mchungaji Damas Ndanda Bukika kuwa katibu mkuu.