Baraka FM

Viongozi wametakiwa kuwa wakweli na kutenda haki ili kulinusuru kanisa, taifa na machafuko

2 April 2026, 10:34

‎Askofu wa kanisa la Moravian Tanzania mhashamu Conrad Nguvumali Sikombe (picha na Hobokela Lwinga)

Amani ni tunda la roho kibiblia,hivyo kila mtu anaowajibu wa kulinda na kutunza Amani eneo alilopo.

Na Hobokela Lwinga

‎Askofu wa kanisa la Moravian Tanzania mhashamu Conrad Nguvumali Sikombe ameongoza ibada  ya maombi ya kuliombea taifa.

‎Ibada hiyo imefanyika katika kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi ushirika wa Nzovwe jumapiili machi 29,2026.

‎katika ibada hiyo askofu Sikombe amesema taifa limepotoka linahitaji rehema za Mungu iwe kwa viongozi,kanisa na taifa kwa ujumla.


‎Katika hatua nyingine amesema taifa linapokosa amani husababisha shughuli za maendeleo kusimama iwe ndani ya familia hadi maendeleo ya nchi.

‎Sambamba na hayo amesema viongozi waliopewa nafasi katika uongozi wanapaswa kuwa wakweli na kutenda haki ili kulinusuru kanisa,taifa na machafuko.

‎Aidha katika mahubiri yake amesistiza waumini kuishi maishi matakatifu yanayompendeza Mungu ikiwa ni pamoja na kutenda mema.

‎Askofu wa kanisa la Moravian Tanzania mhashamu Conrad Nguvumali Sikombe(Katikati) kushoto ni mchungaji Jonam Msangawale wa ushirika wa Nzovwe na kulia ni Hobokela Lwinga Mtangazaji Baraka Media.