Baraka FM

King James Pharmacy watoa msaada hospital ya Rufaa kanda Mbeya

9 March 2026, 23:19

Dkt Mbwanji(kulia) akipokea msaada ulio tolewa na Mkurugenzi wa King James Pharmacy, Dkt. Gloria Mbwile(kushoto)

Katika kuadhimisha sikuku ya mama Duniani taasisi ya King James Pharmacy wameamua kutoa msaada wa vifaa vya matibabu katika hospital ya Rufaa kanda ya Mbeya

Na Ezra Mwilwa

King James Pharmacy Yaweka Alama ya Kipekee MZRH, Yaonyesha Kiu ya Wazawa Kuikwamua Sekta ya Afya.

Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya (MZRH), leo imepokea msaada wa vifaa tiba vyenye thamani ya Shilingi Milioni 103 kutoka kwa Uongozi wa King James Pharmacy ya jijini Mbeya katika kuunga mkono juhudi za Serikali katika maboresho ya huduma ya afya nchini.

Baadhi ya vifaa vilivyo tolewa na King James Pharmacy(picha na Ezra Mwilwa)

Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo, Mkurugenzi wa King James Pharmacy, Dkt. Gloria Mbwile ameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Saia Suluh Hassan Rai wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mapinduzi makubwa katika sekta ya afya .

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya Dkt. Godlove Mbwanji ameeleza kufarijika sana na hatua hiyo ya kizalendo.

Baadhi ya watumishi wa King James Pharmacy na hospital ya Rufaa kanda ya Mbeya

Nao watumiaji wa vifaa hivyo, Muuguzi Mkuu wa Hospitali, Petro Semen, pamoja na Seraphine Mushi Mkuu wa Kitengo cha fiziotherapia, wamesema kuwa vifaa hivyo vya kisasa vitaongeza ufanisi na kupanua wigo wa utoaji huduma kwa wagonjwa, huku wakiahidi kuvitunza ili vidumu kwa muda mrefu.

Msaada huo uliotolewa maalum katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani, unajumuisha vifaa muhimu kwa ajili ya Idara ya Tiba kwa Vitendo (Physiotherapy), Wodi ya Watoto, pamoja na Kitengo cha Uangalizi Maalum (ICU).