Baraka FM
Baraka FM
17 February 2026, 15:46

Zao la nyuki linatajwa kuwa na faida mbalimbali za kiafya na kiuchumi.
Na Hobokela Lwinga
Vijana wametakiwa kuchangamkia fursa za ufugaji wa nyuki kwa ajili ya kujiongezea kipato hali itakayopunguza malalamiko ya ukosefu wa ajira nchini.
Rai hiyo imetolewa na mkurugenzi wa kampuni ya GeoAfrrica consultant Lukelo Mgana wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelekea kwenye kongamano la vijana linahusu uzalishaji wa mazao ya nyuki linalotarajiwa kufanyika mwezi machi,mwaka huu.
Sambamba na hayo amesema Zaidi ya vijana 500 watashiriki katika kongamano hilo,mgeni rasmi anatarjiwa kuwa ni waziri wa nchi ofisi ya rais ,maendeleo ya vijana Joel Nanauka na mgeni mwalikwa akiwa ni Waziri mkuu mstaafu Mizengo Peter Pinda.

David Lyama ambaye ni mfugaji nyuki kibiashara mkoani Mbeya na mwakilishi wa kampuni ya ufugaji nyuki TABEDO,amesema sekta ya ufugaji nyuki imeweza kutoa ajira zaidi ya milioni mbili, huku akishauri mamlaka zinazohusika na ufugaji kuendelea kutoa elimu kwa jamii kuhusiana na ufugaji bora wa nyuki.
