Baraka FM

Moravian yapata mradi mpya,kuwagusa wanawake watoto wenye ulemavu na mabinti wanaoishi mazingira magumu

16 February 2026, 19:54

Baadhi ya viongozi wa KMT-JKM walioshiriki katika hafla ya uzinduzi wa mradi wa Gender justice project (picha na Hobokela Lwinga)

‎Kanisa la Moravian Jimbo la kusini magharibi limeendelea kutelekeza miradi mbalimbali inayofadhiliwa na shirika la mission 21.

‎Na Hobokela Lwinga

Kanisa la Moravian Jimbo la kusini magharibi kupitia idara ya udiakonia kwa mwaka 2026 imetambulisha mradi mpya uitwao Gender justice project utaokaofanyika katika shirika za kanisa hilo zilizopo katika halmashauri Mbeya.

‎Akizungumza wakati wa utambulisho wa mradi huo katika ukumbi wa ofisi za Jimbo hilo,afisa mradi upande wa afya Emmanuel angetile amesema mradi huo utakuwa wa mwaka mmoja na nimahususi kwa watu wenye ulemavu.

Afisa mradi upande wa afya KMT-JKM Emmanuel Angetile(picha na Hobokela Lwinga)
Sauti ya Emmanuel Angetile

Aidha ametaja wanufaika wa mradi huo wanawake na watoto wenye ulemavu pamoja na mabinti wanaoishi katika mazingira magumu.

‎Awali akifungua hafla ya ufunguzi wa mradi huo makamu mwenyekiti wa kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi Mchungaji Agnes Njeyo amewataka washiriki kuwa na mawazo chanya wa kusaidia mradi kutimizwa kwa malengo yaliokusudiwa.

Makamu mwenyekiti kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi Mchungaji Agnes Njeyo(picha na Hobokela Lwinga)
Sauti ya Mch Agnes Njeyo

‎kwa upande wake katibu mkuu wa kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi Mchungaji Nsevilwe Msyaliha amewataka wasimamizi wa mradi huo kuufanya kwa uaminifu mkubwa ili kutowakatisha tamaa wafadhili wa mradi.

Katibu Mkuu kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi Mchungaji Nsevilwe Msyaliha(picha na Hobokela Lwinga)
Sauti ya Mchungaji Nsevilwe Msyaliha

‎Hata hivyo mwakilishi wa shirika la mission 21 Isaac Mwakapasya Ameitaka idara ya udiakonia katika kutelekeza mradi huo kuwatumia wataalam kutoka serikani.

Mwakilishi wa shirika la mission 21 Isaac Mwakapasya(picha na Hobokela Lwinga)
Sauti ya Isaac Mwakapasya

Mradi wa Gender justice project utafanywa nchini Tanzania kwa mwaka mmoja na kanisa la Moravian kupitia idara ya udiakonia ukiwa umefadhiliwa na shirika la mission 21 ambalo limekuwa likifadhili miradi mbalimbali katika kanisa.