Baraka FM
Baraka FM
15 February 2026, 18:03

Wachungaji na waumini watakiwa kushirikiana katika ujenzi wa miundombinu ya kanisa kwa hali na mali.
Na Hobokela Lwinga
Mwenyekiti wa kanisa la Moravian wilaya ya Mbeya mchungaji Greenwell Sinkwembe amewataka Wakristo katika wilaya yake kujitoa kwa ajili ya kazi ya Mungu ikiwa ni sambamba na ujenzi wa ofisi za wilaya na nyumba za watumishi.

Kauli hiyo ameizungumza katika ibada ya kumpokea kuanza rasmi kazi katika wilaya ya Mbeya, iliyofanyika katika kanisa la Moravian usharika wa mabatini jijini Mbeya.
Aidha mch.Sinkwembe amewaomba Wakristo kuwa chanzo cha amani na kuepuka migogoro ndani na nje ya kanisa hali itakayosaidia maendeleo mbalimbali ya kanisa na taifa.

Kwa upande wake mwenyekiti wa wilaya ya uyole mchungaji Godfrey Tinga wakati akihubiri amesema kanisa linapaswa kuhubiri amani, kwani amani ni msingi wa mambo mengi.

Akizungumza kwa niaba ya wachungaji wenzake mchungaji Jonam Msangawale amesema wako tayari kuumuunga mkono mwenyekiti wao katika kutekeleza majukumu yake ya ujenzi wa kanisa.