Baraka FM

Mch. Tinga apokelewa rasmi na mwenyekiti Moravian Uyole

9 February 2026, 09:49

Mwenyekiti wa wilaya ya Uyole Kanisa la Moravian Jimbo la kusini magharibi Mchungaji Godfrey Tinga(katikakati)akiwa na mke wake wakisalimiana na Mwenyekiti wa wilaya ya Mbeya mchungaji Greenwell Sinkwembe(kushoto)

Baada ya uchaguzi wa viongozi mbalimbali wakimewo wenyeviti wa wilaya katika kanisa la Moravian Jimbo la kusini magharibi na wewe kisha kupangiwa vituo vya kazi,wilaya ya uyole imempokea mwenyekiti wake.

Na Hobokela Lwinga

Rasmi mwenyekiti wa wilaya ya Uyole Kanisa la Moravian Jimbo la kusini magharibi Mchungaji Godfrey Tinga amepokelewa na kukaribishwa kuanza kuitumikia nafasi hiyo.

Ibada ya ukaribisho,imefanyika katika Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi ushirika wa Ibala uliopo jijini Mbeya ikiongozwa na mwenyekiti wa dinari ya Uyole Mchungaji Luka Mtafya.

Mwenyekiti wa wilaya ya Uyole Kanisa la Moravian Jimbo la kusini magharibi Mchungaji Godfrey Tinga (picha na mwandishi wetu)

Aidha ibada hiyo imehudhuriwa na Mwenyekiti wa Wilaya ya Mbeya, Mchungaji Greenwell Sinkwembe ambaye pia alihubiri.

Mchungaji Sinkwembe katika mahubiri yake alisisitiza umuhimu wa uongozi unaojengwa juu ya misingi ya upendo, unyenyekevu na mshikamano wa waumini,Amewahimiza viongozi na waumini kushirikiana kwa karibu katika kuimarisha huduma za kanisa na kukuza maisha ya kiroho ndani ya jamii.

Mwenyekiti wa Wilaya ya Mbeya, Mchungaji Greenwell Sinkwembe(picha na mwandishi wetu)

Ibada hiyo imehudhuriwa na viongozi wa Wilaya ya Uyole, idara mbalimbali za kanisa pamoja na waumini.