Baraka FM
Baraka FM
13 January 2026, 13:37

Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la misheni Iringa limepandishwa hadhi kutoka kuwa jimbo la misheni Iringa na kuwa jimbo kamili litakaloitwa kanisa la Moravian Tanzania jimbo la Iringa.
Na Hobokela Lwinga
Mkutano mkuu wa siondi ya kwanza kanisa la Moravian Tanzania jimbo la Iringa umemchagua mchungaji Bora Benjamin msola kuwa Mwenyekiti wa jimbo hilo.
Katika mkutano huo uliosimamiwa na askofu mlezi wa jimbo hilo ambaye ni askofu wa kanisa la Moravian Tanzania jimbo la kusini magharibi mch.Robert pangani amemtangaza mch.Msola kuwa mwenyekiti kwa kupata kura 48 kati ya kura 53.

katika hatua nyingine mkutano huo umemchagua mchungaji Nsangalufu Katule kuwa makamu mwenyekiti wa Jimbo La Iringa Kanisa La Moravian.

Mkutano huo pia umewachagua wajumbe wengine wa halmashauri kuu ya jimbo wakiwemo wenyeviti wa wilaya tatu za kanisa za Iringa,Mafinga Na Makambako kwa lengo kuimarisha utendaji kazi ya Mungu ndani ya kanisa huku nafasi ya katibu mkuu ikiachwa wazi kwani ni nafasi ya kuajiriwa.

Kabla ya kuanza kwa uchaguzi askofu wa kanisa la Moravian Tanzania Jimbo La Kusini Askofu Kenan Panja aliwataka wajumbe kuruhusu haki ya mungu itawale ili kanisa lipate viongozi wenye hofu ya Mungu.

Jumla ya wajumbe 53 wakiwepo wachungaji kutoka katika shirika 23 zinazounda kanisa Moravian Tanzania Jimbo La Iringa wameshiriki mkutano mkuu wa kwanza wa jimbo hilo unaofanyika kila baada ya miaka mitano.
