Baraka FM

Mtangazaji wa Baraka media afariki dunia

4 November 2025, 13:06

Picha ya Kelvin Lameck

Uongozi wa Baraka FM unasikitika kutangaza kifo cha Kelvin Lameck ambaye alikuwa akitumikia nafasi ya Mhariri Msaidizi katika kituo chetu cha redio.

Marehemu Kelvin Lameck amefariki dunia tarehe 29 Oktoba 2025, tukio lililowaacha kwa majonzi makubwa wafanyakazi wenzake, marafiki na familia yake.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na uongozi wa Baraka FM, mwili wa marehemu utaagwa katika Kanisa la Moravian Tanzania, Jimbo la Kusini Magharibi – Ushirika wa Nzomve, na maziko yatafanyika tarehe 6 Novemba 2025 katika makaburi ya Iwambi, jijini Mbeya.

Uongozi wa Baraka FM umetoa salamu za rambirambi kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa na wote walioguswa na msiba huu, ukimkumbuka Kelvin kama mtumishi mwaminifu, mchapakazi na mwenye moyo wa upendo kwa watu wote.