Baraka FM

DC Mbeya ahamasisha wananchi kupiga kura October 29, 2025

25 October 2025, 21:34

Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya SACP Benjamin Kuzaga (wa tatu kushoto)akiongoza matembezi (wa tatu kulia) ni Mkrugenzi mtendaji halmashauri ya wilaya ya Mbeya Erica Yegella (Picha na Hobokela Lwinga)

Kupiga kura ni haki ya msingi kwa kila mwananchi alikidhi vigezo ikiwemo umri.‎‎

Na Hobokela Lwinga

‎‎Wananchi halmashauri ya wilaya ya Mbeya wameshiriki matembezi ya pole kwa lengo la kujipongeza kwa ushindi wa mbio za Mwenge kikanda oktoba 14,2025 na kuhimiza wananchi kushiriki kupiga kura uchaguzi mkuu oktoba 29,2025.‎‎

Matembezi hayo yaliyoandaliwa na halmashauri ya wilaya ya Mbeya yameongozwa na kamanda wa jeshi polisi mkoa wa Mbeya SACP Benjamin Kuzaga ambaye alikuwa mgeni Rasmi.‎‎

Akizungumzia uchaguzi mkuu wa oktoba  29, 2025 kamanda Kuzaga amewahakikishia usalama wananchi Mkoani Mbeya na kwamba watakapoona kuna viashiria vya uhalifu wasisite kutoa taarifa huku akisema wamejipanga kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani na utulivu.‎‎

Aidha Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Mbeya Erica Yegella amewahimiza wananchi kujitokeza kupiga kura October 29,2025 ambapo vituo vya kupigia kura vitafunguliwa saa moja kamili asubuhi na kifungwa saa kumi jioni hivyo mbio za pole zitumike kuwakumbusha wajibu wao kwenda kupiga kura.‎‎

Kwa upande wake Abuu Mtoro akizungumza kwa niaba ya vilabu vya mbio za pole ameahidi kujitokeza kupiga kura oktoba 29,2025.

‎‎Wananchi na vilabu mbalimbali vya mchezo wa mbio za pole vimeshiriki mbio hizo zilizoanzia Mlima Reli hadi Uwanja wa Mahubiri na kuhitimishwa kwa mazoezi ya viungo yaliyoandamana na mchezo wa kufukuza kuku pamoja na kukimbia na yai kwenye kijiko.‎‎‎‎‎‎‎