Baraka FM

RPC Mbeya aongoza wananchi mbio za pole

25 October 2025, 16:37

RPC mka wa Mbeya Benjamin kuzaka(picha na Ezra Mwilwa)

kutokana kiongozi mbio za mwenge mwaka huu kuitaja halmashauri ya Mbeya kuibuka washindi wa mbio hizo wamefanya tafrija ya kujipongeza pamoja na wananchi.

Na Ezra Mwilwa

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishina Msaidizi Mwandamizi (SACP) Benjamin Kuzaga ameongoza mbio za pole Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya zilizoandaliwa na Mkurugenzi wa Halmashauri Erica Yegella kwa lengo la kujipongeza kwa ushindi wa mbio za Mwenge kikanda oktoba 14,2025 na kuhimiza wananchi kushiriki kupiga kura uchaguzi mkuu oktoba 29,2025.

Awali Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya Erica Yegella amewapongeza wananchi na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya kufanikisha ushindi huo kwani ni ushindi wa Wilaya Mkoa na Kanda kwa ujumla, pia amewahimiza wananchi kujitokeza kupiga kura.

Sauti ya mkurungezi Erica Yegella

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Benjamin Kuzaga ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya kwa ushindi walioupata Kitaifa.

Akizungumzia uchaguzi mkuu oktoba 29,2025 Kuzaga amewahakikishia usalama wananchi Mkoani Mbeya na kwamba watakapoona kuna viashiria vya uhalifu wasisite kutoa taarifa kwani Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limejipanga kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani na utulivu.

Sauti ya RPC Benjamin Kuzaga

Nao baadhi ya washiriki wamesema nihaki ya Kila mwananchi kujitokeza kupiga kura bila kufanya vitendo vya uvunjifu wa amani.

Mchezo wa kukimbiza kuku ulivyo fanyika (picha na Ezra Mwilwa)
Sauti za baadhi ya washiriki

Wananchi na vilabu mbalimbali vya mchezo wa mbio za pole vimeshiriki mbio hizo zilizoanzia Mlima Reli hadi Uwanja wa Mahubiri na kuhitimishwa kwa mazoezi ya viungo yaliyoandamana na mchezo wa kufukuza kuku pamoja na kukimbia na yai kwenye kijiko.