Baraka FM
Baraka FM
21 October 2025, 22:55

Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi kila baada ya miaka mitano linafanya mkutano mkuu.
Na Hobokela Lwinga
Askofu wa kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi mch.Robert Pangani amewataka wajumbe wa mkutano mkuu wa kanisa hilo” Sinodi”kujiepusha na kampeni za kupata viongozi badala yake wajikite kumuomba Mungu ili kupata viongozi waliokusudiwa na Mungu mwenyewe.

Rai hiyo ameitoa wakati akifungua mkutano mkuu huo wa sinodi unaofanyika katika ukumbi wa wilaya ya Mbeya kanisa, uliopo nanenane jijini Mbeya.

Aidha Askofu Pangani ameyataja baadhi ya mafanikio ambayo kanisa limeyapata kwa miaka mitano iliyopita kuwa kufanikiwa kufungua kituo cha runinga cha Baraka Tv.
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wamesema matarajio yao ni kupata viongozi wenye hofu ya Mungu na kuhakikisha kanisa linasonga mbele kiroho na kimwili.

Mkutano huo wa sinodi huwa unafanyika kila baada ya miaka mitano lengo likiwa ni kufanya tathimini ya maendeleo mbalimbali ya kanisa sambamba na kupata viongozi wapya wanaochaguliwa na wajumbe wa mkutano.
