Baraka FM

Dkt. Mpango: Wananchi tudumishe amani, tumuenzi baba wa taifa

15 October 2025, 09:28

Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt.Philip Mpango akihutubia katika kilele cha mbio za mwenge kitaifa 2025 jijini Mbeya.

Mbio za mwenge kitaifa kitaifa 2025 zimehitimishwa rasmi mkoani Mbeya baada kukimbizwa kwa siku 195 nchi nzima.

Na Hobokela Lwinga

Makamu wa Rais Tanzania mhe.Philip Mpango amewataka wananchi wakiwemo vijana kuhakikisha ‎Wanasimamia misingi iliyoachwa na baba wa taifa mwalimu Julias Kambarage Nyerere ikiwa ni pamoja na kulinda uhuru wa taifa, haki,amani, kuimarisha maadili pamoja na kuwajibika katika kuchangia kukua kwa pato la Taifa.

‎‎Makamu wa Rais ameyasema hayo akimwakilisha Rais samia katika kilele cha mbio za mwenge kitaifa zilizoambatana na kumbukizi ya kifo cha baba wa taifa la Tanzania mwalimu Julias Kambarage Nyerere zilizofanyika Katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.‎‎

Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akikabithiwa mwenge wa Uhuru na kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Ismail Ally ussi ishara ya kuhitimishwa katika kilele cha mbio za mwenge kitaifa 2025 jijini Mbeya.
Sauti ya Makamu wa Rais Tanzania mhe.Philip Mpango.

Kwa upande wake Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemwagiza katibu mkuu ofisi ya waziri Mkuu Sera, Bunge na uratibu  kuandaa maudhui ya urithi yanamuhusisha baba wa taifa mwalimu Julias Kambarage Nyerere ili kuyaweka kwenye maktaba na vyuo mbalimbali ili yaweze kusomwa na wananchi kwa lengo la kuelewa falsafa zake.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akihutubia katika kilele cha mbio za mwenge kitaifa 2025 uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Sauti ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

Aidha Waziri wa nchi , Ofisi ya Waziri mkuu,Kazi vijana ,Ajira wenye ulemavu Ridhiwani Kikwete ameeleza mafanikio ya miaka 61  ya mbio za mwenge Kwa Mwaka 2025  ambapo Mwaka huu mwenge wa uhuru umekimbizwa katika mikoa 31 na kuzindua miradi 1382 na kuweka mawe ya msingi katika sekta mbalimbali.‎‎

Picha ya pamoja kati ya viongozi Serikali na wakimbiza mwenge kitaifa
Sauti ya Waziri wa nchi , Ofisi ya Waziri mkuu,Kazi, vijana ,Ajira wenye ulemavu Ridhiwani Kikwete.

Kwa upande wake kiongozi mbio za mwenge wa uhuru kitaifa Ismail Ally Ussi wakati akisoma Risala ya utii amewapongeza viongozi wa mikoa yote 31 na halmashauri zao Kwa ushirikiano waliouonyesha katika kutembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa katika mikoa Yao huku akieeleza kuwa baadhi ya viongozi wa mikoa wamekuwa wakikataa baadhi ya miradi isiweze kutembelewa na Mwenge wa uhuru Kwa dhana ya kwamba miradi hiyo ni mikubwa hivyo itatembelewa na viongozi wa ngazi za juu mara baada ya kutembelea katika mikoa yao.‎

Baadhi ya wananchi waliojitokeza katika kilele cha mbio za mwenge wa uhuru kitaifa jijini Mbeya
Sauti ya kiongozi mbio za mwenge wa uhuru kitaifa Ismail Ally Ussi