Baraka FM
Baraka FM
14 October 2025, 08:04

kuelekea kilele cha mbio za mwenge wa Uhuru na kumbukizi ya kifo cha baba wa Taifa Mwl Julius Nyerere mwakamu wa rais mgeni rasmi mkoani Mbeya.
Na Ezra Mwilwa
Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango, ashiriki Ibada katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Fransisco wa Asili, Mwanjelwa mkoani Mbeya.
lbada maalumu ya kumuombea Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Pamoja na kushiriki lbada hiyo, leo Oktoba 14, 2025, Makamu wa Rais atakuwa mgeni rasmi kwenye kuhitimisha Wiki ya Vijana Kitaifa ambayo maonesho yake yalikuwa yakifanyika katika Viwanja vya Uhindini, Mbeya.

Baadae atashiriki kwenye sherehe za kilele cha mbio za Mwenge na kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa katika Viwanja vya Sokoine, Mbeya.