Baraka FM
Baraka FM
13 October 2025, 19:41

Serikali imeendelea kushirikiana na sekta binafsi na wewe jamii Kukabiliana na maafa.
Na Hobokela Lwinga
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amezitaka wizara na taasisi za kisekta kutenga bajeti kwa ajili ya maafa huku sekta binafsi zikitakiwa kuwa na uwekezaji stahimilivu juu ya majanga ikiwemo uwekaji wa bima na utekelezaji wa miongozo ya serikali.
Waziri Mkuu kuu Majaliwa ameyasema hayo katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kupunguza maafa kitaifa yaliyofanyika katika ukumbi wa city park mkoani Mbeya yakiwa na lengo la kuhamasisha Serikali,wadau na jamii katika makabiliano ya maafa.
Aidha Amesema Serikali imeendelea kuboresha na kuimarisha miundombinu bora sekta za afya,maji ,kilimo lengo likiwa ni Kukabiliana na maafa.
Sambamba na hayo waziri Mkuu Majaliwa amesema Serikali imeendelea kuchukua hatua mbalimbali madhubuti za kuimarisha ustahimilivu wa Taifa juu ya majanga kupitia utekelezaji wa fedha, Sheria, mikakati na miradi mbalimbali.

Kwa upende wake Waziri ofisi ya waziri Mkuu sera,Bunge na uratibu mhe.William Lukuvi amesema katika utekelezaji wizara imeendelea kuratibu utoaji wa mafunzo kwa wataalam katika mikoa na jamii wakiwemo vijana kuhusu usimamizi wa maafa hususani katika hatua ya kuzuia na kujiandaa Kukabiliana na maafa yanapotokea.
Awali akizungumza kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Mbeya Mhe.Beno Malisa, Mkuu wa wilaya ya Kyela Josephine Manase ameishukru serikali kwa kuendeleza maendeleo kwa vijana sambamba na hayo amewahimiza vijana kutumia fursa zinazopatikana mkoani Mbeya.

Katika maadhimisho hayo yaliyofanyika kitaifa katika mkoa wa Mbeya yanakwenda na kauli mbiu “Isemayo wekeza Katika ustahimilivu na si maafa”.