Baraka FM

Rufaa Mbeya yazindua kliniki afya ya akili

12 October 2025, 17:41

Tukio la uzinduzi lilivyo fanywa(picha na Lukia Chasanika)

Katika kuendelea kusogeza huduma kwa jamii, Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya imezindua Kliniki maalumu ya Ustawi na Utimamu wa Afya ya Akili kwa watoa huduma wa Afya Nyanda za Juu Kusini.

Na Lukia Chasanika

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kliniki hiyo Mkurgenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya Dkt. Godlove Mbwanji amewapongeza watumishi wa idara ya Afya na Magonjwa ya Akili kwa hatua hiyo.

Mbwaji amesema watoa huduma wa afya wamekuwa wakitoa huduma kwa watu wengine huku wakisahau kuwa kutokana na maisha ya kila siku inafika wakati hata watoa huduma ya afya nao wanahitaji kupatiwa huduma kama watu wengine.

Sauti ya Dkt. Godlove Mbwanji

Aidha Dkt. Mbwanji amesisitiza kuwa ni muhimu kubadilisha msimamo katika jamii kwani watu wengi huzani kuwa mtu mwenye changamoto ya akili ni yule anayeokota makopo jambo ambalo si kweli kwani mtu hadi kufikia hatua hiyo huwa kuna viashiria vya awali ambavyo watu wengi hupitia lakini hawakutambua mapema.

Sauti ya Dkt. Mbwanji

Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Afya na Magonjwa ya Akili Dkt. Beatrice Thadei ambaye pia ni Daktari Bingwa wa Afya na Magonjwa ya Akili amesema, watumishi wa afya wamekuwa wakikumbana na changamoto mbalimbali za kimaisha kama watu wengine,hivyo kupelekea kupata changamoto ya afya ya akili.

Sauti ya Dkt. Beatrice Thadei

Dkt Beatrice amesema kliniki hiyo itakuwa mahali pa uponyaji, tumaini na uelewa itakayotoa ushauri, matibabu kutoka kwa wataalam waliobobea na kusisiza kuwa kutafuta msaada sio ishara ya udhaifu bali ni kujitambua.

Sauti Dkt. Beatrice Thadei

Mashirika mbalimbali yasiyo ya kiserikali nchini ikiwemo shirika la DSW Tanzania kupitia mradi REST wameendelea kutoa elimu kwa vijana juu afya ya akili ili kunusuru wimbi la vijana kupata ugonjwa huo kwani vijana ni taifa la leo na kesho.Sauti ya mkurugenzi shirika la DSW Tanzania Peter Owaga

Sauti ya Peter Owaga