Baraka FM

Kanisa la Moravian jimbo la Mbozi lapata askofu wa kwanza

8 October 2025, 22:30

Askofu mteule kanisa la Moravian Tanzania jimbo la Mbozi mch.Julias Sikana

Kanisa la Moravian Tanzania kupitia majimbo yake limekuwa na mikutano mikuu ambayo hutoa fursa ya kufanya uchaguzi wa kidemokrasia kupata viongozi.

Na Hobokela Lwinga

Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la limefanya mkutano Mkuu (sinodi)na kufanikiwa kupata askofu wa kwanza katika jimbo hilo.

‎Askofu mteule katika jimbo hilo ni mchungaji Julias Sikana ambaye amepata kura 257 kutoka kwa wajumbe wa mkutano huo.

‎Aidha viongozi wengine waliochaguliwa ni mchungaji Lawrence Nzowa ambaye amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Jimbo,mch.Laison Kibona kuwa makamu mwenyekiti na mch.Japhet Nyangwa kuwa  Katibu Mkuu.

‎Mkutano huo wa sinodi ni wa pili kufanyika tangu Jimbo hilo kuanzishwa.