Baraka FM

Wahitimu kidato cha nne washauriwa kuwa makini katika vyumba vya mitihani

6 October 2025, 16:47

Wanafunzi wahitimu kidato cha nne katika shule ya Sekondari Izuo(picha na Lukia Chasanika)

Umakini wa Mwanafunzi wakati wa kufanya mtihani ndio sababu kubwa ya kufanya vizuri.

‎‎Na Lukia Chasanika‎‎

Wahitimu ya kidato cha nne katika shule ya sekondari Izuo wameshauriwa kuwa makini katika vyumba vya mitihani ili kufanya vizuri katika mitihani yao.‎‎

Ushauri huo umetolewa na mwalimu mstaafu Nazareth Mwaigaga akiwa mgeni rasmi katika mahafali ya sita katika shule ya sekondari Izuo iliyopo kata ya Iyunga mapinduzi katika halmashauri ya wilaya ya Mbeya mkoani Mbeya.‎‎

Mwaigaga amesema wanafunzi hao wanatakiwa kuwa wavumilivu katika masomo yao kabla na baada ya kufanya mitihani yao kwa kutosikiliza maneno ya watu kuwa hakuna ajira kwani serikali ya awamu ya sita inawajali wanafunzi kwa kuwapatia mikopo ya elimu ya juu.‎‎

Aidha katika mahafali hiyo Mwaigaga ametoa vifaa mbalimbali kwa ajili ya walimu kufundishia ikiwemo chaki, karatasi kwa ajili ya kuchapishia mitihani na peni za kusaishia kazi za wanafunzi.‎‎

Mwalimu mstaafu Nazareth Mwaigaga akiwa mgeni rasmi(picha na na Lukia Chasanika)
Sauti ya mwalimu mstaafu Nazareth Mwaigaga akiwa mgeni rasmi

Kwa upande wa mwalimu mkuu wa shule ya sekondari Izuo Efraim Nyamba amesema wanafunzi wanaohitimu kwa mwaka 2025 katika mahafali ya sita ni 59 ikiwa wakiume ni 28 na wakike ni 31 huku akisema shule hiyo iko vizuri kitaaluma.

Mwalimu mkuu wa shule ya sekondari Izuo Efraim Nyamba (picha na Lukia Chasanika)

‎‎Aidha amewaomba wazazi kuwapeleka katika shule hiyo kutokana na ada yake kuwa chini ukilinganisha na shule zingine na ametoa sababu za ada kutofautiana kati ya wavulana na wasichana kuwa mmiliki wa shule hiyo anatamani kuwainua watoto wa kika zaidi kutokana na wazazi wengi kutowasomesha watoto wa kike.‎‎

Sauti ya mwalimu mkuu wa shule ya sekondari Izuo Efraim Nyamba

Wakisoma lisara kwa mgeni rasmi wahitimu wamesema kwa muda waliokuwepo shuleni hapo wamefanikiwa kulima mahindi ambayo yamewasaidia kununua mashine ya kuchapishia mitiani pamoja na kushiriki kufanya usafi katika zahanati na ofisi ya kijiji huku wakieleza kuwa changamoto kubwa ni ushiriki mdogo wa wazazi katika kuwapeleka shuleni hapo.

Sauti za wanafunzi wahitimu

‎‎Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi na mlezi wa shule Willium Mwaweza amewataka wazazi wa kata ya iyunga mapinduzi kuwa na mwamko wa kuwapeleka watoto shule ya sekondari izuo kwani ipo karibu na maeneo wanakotoka watoto.

Sauti ya mwenyekiti wa bodi na mlezi wa shule Willium Mwaweza