Baraka FM

Askofu Pangani ashiriki ibada uzinduzi kanisa la Moravian Forest mpya

25 September 2025, 14:13

Sehemu ya muonekano wa kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi ushirika wa Forest mpya (picha na Hobokela Lwinga)

Mungu anapendezwa na wewe watu wanaojitoa kufanya kazi yake duniani ukisoma Kitabu kitakatifu cha Biblia Hagai 1:8 inasema “Pandeni milimani, mkalete miti, mkaijenge nyumba; nami nitaifurahia, nami nitatukuzwa, asema BWANA.”

‎Na Hobokela Lwinga

‎Zaidi ya shilingi milioni 380 zimetumika katika ujenzi wa majengo mbalimbali ikiwemo ujenzi wa jengo la kuabudia katika kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi ushirika wa Forest mpya jijini Mbeya.

‎Akisoma taarifa ya ujenzi katika ibada ya Uzinduzi wa jengo la kuabudia katika ushirika wa Forest mpya, mchungaji wa ushirika huo Alfred Kashililika amesema fedha hizo zimetokana na waumini pamoja na wadau mbalimbali.

Sauti ya mchungaji wa ushirika wa Forest mpya mch.Alfred Kashililika

‎Aidha mch.Kashililika ameongeza kuwa ushirika huo ulianza January 2021 ukiwa na waumini 84 na mpaka sasa unazinduliwa una waumini 226 ikiwa ni idadi ya watoto na watu wazima.

Sauti ya mchungaji wa ushirika wa Forest mpya mch.Alfred Kashililika
Baadhi ya waumini wa kanisa la Moravian ushirika wa Forest mpya(picha na Hobokela Lwinga)

‎Nae Mwenyekiti wa kamati ya Uzinduzi Hulimboka Tuntufye Mwandoloma amewashukru wote walishiriki na kufanikisha ibada hiyo ya Uzinduzi wa jengo la kuabudia.

‎Akiwa mgeni rasmi katika Uzinduzi wa jengo hilo, askofu wa wa kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi mch.Robert Pangani amesema kukamilika kwa kazi hiyo ya ujenzi anapaswa kushukriwa Mungu huku akiwataka wote walishiriki kutokuwa na roho ya kujisifu.

Askofu Robert Pangani wa KMT-JKM(kulia akiongoza ibada ya Uzinduzi wa kanisa la Moravian Forest Mpya na kushoto ni viongozi wengine wa jimbo na wilaya (Picha na Hobokela Lwinga)