Baraka FM
Baraka FM
16 September 2025, 07:26

Kutokana na kuwepo wa gharama kubwa katika matibabu ya macho, shirika la Helen Keller International limejitoa kusaidia watu wenye tatizo la macho mkoani Songwe.
Na Ezekiel Kamanga
Katika hatua muhimu ya kupunguza upofu unaepukika, Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya (MZRH) na Shirika Helen Keller International leo wamewasili mkoani Songwe kwaajili ya kutoa Huduma Mkoba ya matibabu ya ugonjwa wa mtoto wa jicho
Dkt. Jofrey Josephat Mratibu wa Huduma za macho Mkoa wa Songwe ameeleza kuwa kambi hiyo ya siku 6 imelenga kukabiliana na magonjwa ya mtoto wa jicho vilevile kusogeza huduma hizo karibu na wananchi.

Dkt. Barnabas Mshangila, Daktari Bingwa wa Macho kutoka Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya, ameeleza kuwa huduma hiyo ya matibabu ya upasuaji ya mtoto jicho inawezesha kurudisha nuru kwa mtu ambaye alikua haoni na kuweza kuona tena.
Nao Edward Mkoko na Ericka Mzihowakazi wa mkoa wa songwe waliojitokeza kupata huduma za matibabu hayo, wameishukuru Serikali, Wataalamu wa macho na waandaji wa kambi hiyo kwa kuwasogezea huduma hiyo karibu na maeneo yao bila malipo au gharama nyinginezo.

Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya kwa kushirikiana na Helen Keller International wamejiandaa kuendesha kambi ya siku 6 ya upasuaji wa mtoto wa jicho katika Hospitali ya Wilaya ya Mbozi ambapo inatarajiwa wananchi zaidi ya 700 wafanyiwa matibabu ya upasuaji wa mtoto wa jicho.