Baraka FM
Baraka FM
11 September 2025, 18:02

Wanadamu wametakiwa kujachungu njia nyembamba itakayo wasaidia kuurithi ufalme wa mbinguni siku ya mwisho.
Na Ezra Mwilwa
Askofu wa kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Kusini Magharibi Mch. Robert Pangani amewataka wakristo na watu wote kuchagua njia njema inayompendeza mungu ili waweze kurithi ufalme wa mbinguni.
Rai hiyo katika Ibada ya mazishi ya MCH Ambakisye Ngonya iliyofanyika katika kanisa la Moravian Ushirika wa ZZK uliopo mji mdogo wa mbalizi mkoani Mbeya.

Mch Laurence Nzowa mwenyekiti wa kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Mbozi na Mch Luka Kamwela katibu wa wilaya ya Mbalali Wamesema enzi za uhai wa Mch Ngonya amelitumikia kanisa kwa kuanzisha miradi mbalimbali.

Raphael Mlwafi kwa niaba ya familia na ukoo wa Ngonya amewashukuru viongozi wa kanisa na watu wote walio shiriki katika safari ya kumsindikiza mpendwa wao.
