Baraka FM
Baraka FM
10 September 2025, 10:57

Maisha ya Duniani ni mafupi sana ni vyema kuishi maisha ya kumpendeza Mungu kwani hakuna mtu anayejua mwisho wake duniani.
Na Hobokela Lwinga
Mchungaji mstaafu Ambakisye Ngonya wa kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi amefariki Dunia.
Taarifa iliyotolewa na makamu mwenyekiti kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi mch.Asulumenie Dickson Eva Mwahalende imesema marehemu amefariki wakati anapatiwa matibu katika hospitali ya UWATA Mbeya.
Mch.Mwahalende amesema ibada ya mazishi itafanyika Alhamis September 11,2025 katika ushirika wa ZZK uliopo mji mdogo wa Mbalizi mkoani Mbeya na amesema marehemu atazikwa huko kwani ndiko alikokuwa akiishi enzi za uhai wake.
Aidha amesisitiza kuikumbuka familia kwa sala na maombi katika kipindi hiki kigumu ambacho inapitia.