Baraka FM
Baraka FM
29 August 2025, 19:44

kutokana nauwepo wa magonjwa mbalimbli yakuambukiza na yasiyo yakuambukiza vijana wamehimizwa kwenda kufanya vipimo vya Afya zao
Na Ezra Mwilwa
Wanafunzi waliopo vyuoni wahimizwa kuto kujihusisha na vitendo viovu vinavyo weza kuwasababishia kupata maambukizi ya virusi vya UKIMWI
Wito huo umetolewa na wakufunzi wa kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi kupitia Idara ya Udiakonia Lulu Mpenja na Bitrice Mwakipesile waliopo kuwa wakitoka Elimu ya kujikinga na maambukizi ya UKIMWI kwa wanafunzi MVTC kadege.

Nao baadhi ya wanafunzi walio shiriki katika mafunzo hayo wamesema watahakikisha Wana tekeleza mafunzo yote waliyo pewa.

Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi kupitia Idara ya Udiakonia wameendelea kutoa mafunzo hayo kwa wafanyakazi na wanafunzi wa taasisi zote za kanisa.