Baraka FM

Moravian yaadhimisha siku ya kushukiwa na Roho Mtakatifu

13 August 2025, 21:10

Viongozi wa ibada wakiongozwa na makamu mwenyekiti KMT-JKM mch.Asulumenye Mwahalende na wakristo washiriki katika ibada ya kushuka kwa Roho Mtakatifu (picha na Hobokela Lwinga)

Historia inaonyesha kuwa kanisa la Moravian ndilo kanisa la pili kuanzishwa na la Kwanza duniani kuanzisha uamsho likitokea kanisa catholic.‎‎

Na Hobokela Lwinga ‎‎

Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi limeungana na wakristo wa dhehebu hilo kuadhimisha siku ya kushuka Roho mtakatifu kwa kanisa hilo ibada iliyofanyika kijimbo katika ushirika wa Ruanda jijini Mbeya.‎‎

Ibada hiyo imeongozwa na makamu mwenyekiti wa kanisa la Moravian Tanzania jimbo la kusini magharibi mch. Asulumenye mwahalende imefanyika leo august 13 ,2025 na imehudhuriwa na mchungaji Osia mbotwa mwenyekiti wilaya ya Mbeya na mch. Erica Mwanijembe mwenyekiti wilaya ya Mbalizi.

‎‎Wageni wengine walioshiriki ibada hiyo ni katibu mkuu mstaafu wa kanisa la Moravian Tanzania jimbo la kusini magharibi mch.Daudi Malimali Nsweve,Mwingine Ni Katibu Wa Idara Ya Uwakili Mch.Paul Mwambalaswa.‎‎

kwa upande wake makamu mwenyekiti wa kanisa la Moravian Tanzania mchungaji Asulumenye mwahalende ametumia fursa hiyo kuwashkru watu wote walishiriki ibada hiyo huku akisema kushuka kwa Roho Mtakatifu kwa kanisa hilo ndio mwongozo ambao kanisa linatembea nao mpaka sasa.

‎‎Kwa upande wake mwenyekiti wa kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi wilaya ya Mbeya mch.Osia Mbotwa amesema ni jambo jema kanisa kufuatilia historia kuhusu mwanzo wake na kule linakokwenda.‎‎

Akihubiri kwa kutoa historia ya katika ibada hiyo, katibu Mkuu mstaafu kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi mch.Daudi Nsweve amesema baada ya Roho Mtakatifu kulishukia kanisa la moravian huo ndio ulikuwa mwanzo wa kanisa hilo kuenea kwa wingi duniani.‎‎

Aidha katika ibada hiyo pia imefanyika ibada ya ushirika Mtakatifu kwa wakristo wote washiriki.

Makamu mwenyekiti KMT-JKM mch.Asulumenye Mwahalende akiongoza ibada ya ushirika Mtakatifu (picha na Hobokela Lwinga)

‎‎Ikumbukwe kuwa ushiriki wa ibada hiyo ‎Ni kukumbuka ibada ya ushirika Mtakatifu iliyofanyika august 13,1727 huko Herrnhurt Ujerumani ambapo baada ya ibada hiyo Roho Mtakatifu aliwashukia washiriki.

Wakristo wakishiriki ibada ya ushirika Mtakatifu (picha na Hobokela Lwinga)