Baraka FM

Kanisa la Moravian kufanya ibada ya kushuka Roho Mtakatifu

4 August 2025, 14:22

Kaimu Katibu Mkuu kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi mch.Nsevilwe Msyaliha (kushoto).

Ibada ni sehemu ya maisha ya binadamu, hivyo kila mtu anaowajibu wa kuheshimu ibada katika maisha.

Na Hobokela Lwinga

Kanisa la Moravian Tanzania limetoa taarifa ya uwepo wa ibada ya kukumbuka kushuka kwa Roho mtakatifu itakayofanyika August 13,2025 katika shirika zake zote.

‎Akitoa taarifa ya ibada hiyo Kaimu katibu Mkuu kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi mchungaji Nsevilwe Msyaliha amesema ibada hiyo ni kumbukumbu ya kushuka Roho Mtakatifu baada ya ushiriki wa ushirika Mtakatifu Herrnhurt Ujerumani August 13,1927.

‎Taarifa ya Katibu Mkuu huyo inasisitiza kuwa kwa kila mchungaji aliyepo kwenye ushirika kutoa huduma ya ushirika Mtakatifu huku kila mkristo kuendelea kuombea ibada hiyo.

‎Sambamba na hayo mchungaji Msyaliha amesema ibada ya jimbo itafanyika katika kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi ushirika wa Ruanda Mbeya.