Baraka FM

Ajali yaua wanafunzi 6 wakikimbia mchakamchaka Mbeya

26 July 2025, 16:08

Baadhi ya wananchi wakiwa eneo ilipotokea ajali

Matumizi mabaya ya barabara pasipo kufuata sheria za barabarani husabisha athali ikiwemo ajali.

Na Hobokela Lwinga

Wanafunzi sita wa Sekondari ya Chalangwa Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya wamefariki kwa kugongwa na basi lenye namba za usajili T DCE 194 YUTONG linalomilikwa na Kampuni ya Safina linalofanya safari zake Lualaje Mbeya majira ya saa 11:30 alfajiri barabara kuu ya Chunya Mbeya.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya ACP Wilbert Siwa amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambapo wanafunzi watano wamefariki papo hapo na mmoja amefariki akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Chunya na majeruhi tisa wamepokelewa Kituo cha Afya Chalangwa.

Siwa amesema mara baada ya tukio dereva wa basi hilo alitoroka na juhudi za kumtafuta zinaendelea ambapo ametoa wito kwa madereva kuwa waangalifu wawapo barabarani na chanzo kikitajwa ni mwendo kasi na uzembe wa dereva.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya ACP Wilbert Siwa
Sauti ya Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya ACP Wilbert Siwa

kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Chunya alhaji Mbarack Batenga amepiga marufuku kwa shule au vikundi vyovyote kufanya mazoezi barabarani.

Mkuu wa wilaya ya Chunya alhaji Mbarack Batenga
Sauti yamkuu wa wilaya ya Chunya alhaji Mbarack Batenga

Mganga mfawidhi katika kituo cha afya chalangwa dkt Henry sifuraiton amesema majira ya saa kumi na mbili asubuhi walipokea maiti za wanafunzi watano na majeruhi nane ambapo hali za majeruhi zinaendelea vizuri mpaka sasa.

Mganga mfawidhi katika kituo cha afya chalangwa dkt Henry sifuraiton
Sauti ya Mganga mfawidhi katika kituo cha afya chalangwa dkt Henry sifuraiton

Aidha mkuu wa shule ya Sekondari Chalangwa pamoja na majeruhi katika ajali hiyo wamesema wamekuwa na mazoea ya kufanya mazoezi kila Jumamosi lengo likiwa ni kuimarisha afya zao.

Mkuu wa shule ya Sekondari Chalangwa
Sauti za mkuu wa shule ya Sekondari Chalangwa pamoja na majeruhi