Baraka FM

Ask. Pangani azindua shule Moravian Mwangaza Academy

26 July 2025, 07:25

Askofu Robert Pangani  wa kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi akijiandaa kukataa utepe kiashiria cha Uzinduzi rasmi shule Moravian Mwangaza Academy.

Maendeleo ya elimu yanategemea mchango mbalimbali wa wadau wanaojitikeza kuwekeza katika sekta hiyo.‎‎

Na Hobokela Lwinga

Askofu Robert Pangani  wa kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi amezindua rasmi shule Moravian Mwangaza Academy inayopatikana katika jimbo la mission mkoani Iringa.‎‎

Hafla hiyo imefanyika 18 Julai 2025 na ilihudhuriwa na  uwepo wa familia ya Gobel, wakiwakilisha HMH Ujerumani, ambao ni wafadhili na wamewezesha kukamilika kwa mradi huo.

Sambamba na wageni hao pia Uzinduzi huo ulipambwa maonyesho ya Kitamaduni, Kwaya za wenyeji na vikundi vya ngoma.‎‎

Aidha katika uzinduzi huo Askofu Pangani aliongoza maombi na kuachilia baraka kwa shule hiyo na kwa wageni mbalimbali walifika kushuhudia.‎‎

Mradi huu umesimamiwa na Tanzania Mwangaza, shirika lisilo la kiserikali linalojishughulisha na maendeleo ya jamii na elimu inayojumuisha watu wote.‎‎

Hata hivyo Shule hiyo inatarajia kuhudumia wanafunzi wa nje na ndani ya mkoa Wa Iringa kwa kuzingatia ubora wa masomo na ukuaji wa kwa ujumla. 

‎‎Ikumbukwe kuwa Uzinduzi huu unaashiria ushirikiano imara kati ya jamii za Tanzania na marafiki wa kimataifa walioungana kwa ajili ya mabadiliko kupitia elimu.‎‎