Baraka FM

Moravian Mbeya kuwezesha kwaya kuelekea Sinodi

19 July 2025, 08:42

kiongozi wa umoja wa vijana kati Dinari ya Mbeya Hezron Ngoya akitoa taarifa ya utendaji kazi ya miaka minne ya uongozi wake katika dinari ya Mbeya mjini (picha Hobokela Lwinga)

Kama ilivyo desturi ya Kanisa la Moravian Tanzania kuwa na uratibu wa mikutano kuanzia ngazi ya dinari,wilaya,jimbo na KMT kwa kufanya mikutano yake kwenye dinari, mikutano hii inafanyika kila mwaka

‎‎Na Hobokela Lwinga ‎‎

Vijana kati Dinari ya Mbeya kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi imefanya mkutano wao wa mwisho 2025 kuelekea mkutano wa sinodi ambayo unaotarajiwa kufanyika mwezi October.‎‎

Vijana kati ushirika wa Meta wakimtukuza Mungu katika mkutano wao unaofanyika ushirika wa Mbeya mjini(picha na Hobokela Lwinga)

Mkutano huo unafanyika katika kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi ushirika wa Mbeya mjini ndani ya mkoa wa Mbeya.‎‎

Akitoa taarifa ya utendaji kazi wa viongozi wa idara hiyo, kiongozi wa umoja wa vijana kati Dinari ya Mbeya Hezron Ngoya ametaja mafanikio waliyoyafanya kwa miaka minne kuwa ni pamoja na kushirikiana kwa kuchangiana fedha kiasi cha shilingi million moja na laki nane kwa idara ya vijana kati katika shirika zinazounda dinari hiyo.‎‎

Vijana kati ushirika wa Mbeya mjini wakiimba kwenye mkutano wao unaofanyika ushirikani hapo (picha na Hobokela Lwinga)

Aidha amezitaja baadhi ya changamoto ambazo wamekutana nazo katika utendaji wa kazi hiyo ya Mungu kuwa ni vijana wengi kutokuhudhuria mazoezi ya kwaya ya dinari kujiandaa na mikutano na baadhi ya viongozi kutokuhudhuria vikao.

‎‎Ikumbukwe kuwa dinari ya Mbeya kwa Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi wilaya ya Mbeya inaundwa na shirika za Mbeya mjini, Mabatini, Jakaranda (cathedral), Meta, Itiji, Nzovwe na Halengo.