Baraka FM
Baraka FM
9 July 2025, 15:18

Jukumu la kuwasaidia wahitaji ni la kwetu sote pasipo kuchagua dini rangi au kabila la mtu.
Na Hobokela Lwinga
Askofu wa kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi Mchungaji Robert Pangani Ameitaka jamii kutoa faraja kwa kuwasaidia watu wenye ulemavu kwa kuwapa fursa mbalimbali zinazopatikana ili kuwapunguzia changamoto zinazowakabilli.
Rai hiyo imeitoa wakati akifungua semina ya udiakonia katika ukumbi wa hostel za kanisa hilo zilizopo Jakaranda Mbeya mjini,ikiwa imehusisha wadau,watu wenye ulemavu,na baadhi ya viongozi wa idara, Wilaya katika kanisa hilo iliyofadhiriwa na mission 21.
Aidha askofu Pangani amewataka washiriki wote ambao wamefikiwana kupatiwa elimu na kanisa hilo kuitumia vyema ili ziweze kuwasaidia kuondokana na changamoto walizonazo.
Kwa upande wake mratibu wa shirika la mission 21 Tanzania Adriane Sweetman amesema mikakati ya shirika hilo ni kuhakikisha wanawasaidia watu wote ikiwemo watu wenye ulemavu hasa katika kutoa huduma za afya,uchumi na elimu.

Mchungaji Amos Mwampamba ni mwenyekiti wa wilaya ya Mbarali na mchungaji Osia Mbotwa mwenyekiti wa wilaya ya Mbeya kanisa la Moravian Amesema zamani watu walikuwa na mtazamo hasi wakidhani kupata mtoto mwenye ulemavu ni laana na mikosi huku wakisema hali hiyo kwa sasa haipo tena.
Baadhi ya washiriki katika semina hiyo wamesema elimu iendelee kutolewa hasa kwa wanaume kwani wamekuwa waoga kuwahudumia watu wenye ulemavu pindi wanapopatikana kwenye familia zao.
