Baraka FM
Baraka FM
3 July 2025, 19:38

Kujichukulia sheria ni kosa la jina kwa mjibu wa sheria za nchi,na ndio maana wasimamizi wa sheria wamekuwa wakisisitiza wanapobaini uwepo wa waharifu kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Na Hobokela Lwinga
Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Neema Jonas Mkazi wa Kijiji Cha Inyala wilaya ya Mbeya Mkoani ambeya amefariki dunia baada ya kupigwa na kitu butu kichwani na mume wake chanzo kikiwa ni wivu wa kimapenzi.
Wakizungumza na kituo hiki baadhi ya wananchi ambao ni mashuhuda wamesema baada ya kufika walishuhudia kuona shoka na jeraha kwa marehemu sehemu ya kichwani.

Pamoja na hayo wakazi hao wameishauri jamii kufuata taratibu sahihi za utatuzi wa migogoro.
Hata hivyo Mkuu wa polisi kituo cha Inyala Kamishina Msaidizi wa Jeshi la polisi ASP Christopher Zambi Akiwasisitiza wananchi kutojichukulia Sheria mkononi.