Baraka FM

MNEC Mbeya akanusha kuchukua fomu kugombea ubunge

3 July 2025, 12:52

Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM taifa mkoa wa Mbeya MNEC Ndele Mwaselela(Picha na Hobokela Lwinga)

Baada ya taarifa za uvumi za MNEC Ndele Mwaselela kuchukua fomu za kugombea ubunge,leo amejitokeza hadharani kuzungumza.

Na Hobokela Lwinga

Baada ya zoezi la uchukuaji wa fomu za kugombea udiwani na ubunge ndani ya CCM,Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM taifa mkoa wa Mbeya MNEC Ndele Mwaselela amekanusha taarifa za yeye kuchukua fomu za kugombea ubunge jimbo lolote mkoani Mbeya.

‎Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Chama hicho mkoa wa Mbeya,Ndele Mwaselela amesema yeye ataendelea kuwatumikia wananchi kwenye cheo alichonacho cha U-NEC.

‎Amesema kazi yake kwa sasa ni kuwaunganisha wananchi na kukisaidia chama chake kushinda uchaguzi mkuu ujao unaotarajiwa kufanyika October mwaka huu 2025.‎

‎Katika hatua nyingine ameelezea mafanikio yake ya uongozi tangu alipoingia madarakani katika wadhifa huo kuwa ni pamoja na kuhamasisha ujenzi wa ofisi za chama kuanzia ngazi ya kata hadi wilaya.