Baraka FM
Baraka FM
3 July 2025, 19:10

kufuatia uwepo wa gharama kubwa za matibabu ya macho mbunge wa vitimaalumu mkoa wa Mbeya mhandisi Maryprica Mahundi amelipiwa matibabu kwa mda maalumu ulio pangwa
Na Josea Sinkala
Katika kuboresha huduma za kiafya kwa wananchi, Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ambaye ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mbeya Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi amefungua kambi ya matibabu kwa wagonjwa wa macho katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Mbeya yanayotolewa bure kwa udhamini wa Mbunge huyo kwa kushirikiana na taasisi isiyo ya kiserikali ya MWEF inayoiendesha mkoani Mbeya.

Akizungumza na wananchi waliojitokeza kupata huduma za macho, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi, amesema gharama zote za uchunguzi, dawa na matibabu ni bure kupitia wadau wake kutoka Ujerumani kwa ushirikiano na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya.
Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha macho katika Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Mbeya Dkt. Fariji Kilewa, amesema lengo ni kuwafikia wagonjwa zaidi ya mia mbili katika Mkoa wa Mbeya na maeneo mengine ya jirani.
Dkt. Kilewa amesema mbali ya upasuaji wa mtoto wa jicho pia hospitali na timu ya Madaktari bingwa kutoka nchini ujerumani watawafanyia uchunguzi wa macho juu ya matatizo mbalimbali yahusuyo macho.
Hata hivyo Dkt. Fariji Kilewa amesema gharama za upasuaji wa mtoto wa jicho zinagharimu zaidi ya shilingi laki tatu ambazo ni watu wachache wanaoweza kumudu gharama hizo hivyo kumshukuru Mhe. Mbunge wa viti maalum (Kupitia kundi la Wanawake mkoa wa Mbeya) Mhandisi Mahundi kwa kuwa na moyo wa kujitoa.
Afisa Uhusiano wa Hospitali ya Mkoa wa Mbeya Agrey Mwaijande, amesema gharama zote zinatolewa bure hivyo kuwaasa wananchi kutumia vizuri fursa hiyo vyema kuhakikisha wanajitokeza kupimwa na kutibiwa macho bure.

Baadhi ya wagonjwa waliojitokeza kupatiwa watibabu wamepongeza huduma hiyo kutokana na wengi wao kushindwa kumudu gharama za matibabu ya macho.
Ikumbukwe hii ni kambi ya pili kwa Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi kuandaa kambi ya macho iliyoanza Juni 30, 2025 itakayotamatika julai 5, 2025 Mkoani Mbeya.