Baraka FM
Baraka FM
30 June 2025, 16:33

Wakati jamii ikiwaamini watu wenye elimu ,jamii hiyo hiyo inawataka wenye elimu kuonyesha umuhimu wa elimu waliyoipata.
Na Rukia Chasanika
Wanafunzi wanaohitimu katika vyuo vya maendeleo ya jamii mkoani Mbeya wameshauriwa kuandika maandiko ya miradi mbalimbali ambayo itasaidia kupunguza wimbi la watoto wasio na makazi maalumu mkoani Mbeya.
Wito huo umetolewa katika mahafali ya 12 ya chuo cha maendeleo ya jamii Kaps na mgeni rasmi Devota Chacha aliyemwakilisha mh. Beno malisa aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Mbeya na sasa ndiye mkuu wa mkoa wa Mbeya
Devota amesema kutokana wimbi kubwa la watoto wasio na makazi maalumu ni wakati sasa wa wanavyuo wanaohitimu masomo ya maendeleo ya jamii kutumia fursa hiyo kuandika maandiko mbalimbali ambayo yatawapatia fedha za kuwasaidia watoto hao.
Kwa upande wake mkuu wa chuo cha maendeleo ya jamii KAPS Mbeya Denis Brighton amesema chuo hicho kimetoa viongozi mbalimbali katika taasisi za serikali na binafsi na wengine kujiendeleza vyuo vikuu.
