Baraka FM

Askofu Pangani awataka vijana kutumia ibada za sifa kuishi maisha hekima na kujiinua kiuchumi

29 June 2025, 16:48

Askofu Robert Pangani wa kanisa wa kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi akifungua ibada ya the Joy of Praise (picha na Hobokela Lwinga)

Ukisoma Biblia takatifu kitabu cha Zaburi 66:8 Inasema “Enyi mataifa, mtukuzeni Mungu wetu,Itangazeni sauti ya sifa zake;”

‎‎Na Hobokela Lwinga ‎‎

Askofu wa kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi mch.Robert Pangani amewataka vijana kuishi maisha ya hekima yatakayoleta matokeo chanya ya maisha ya kimwili na Kiroho.

‎‎Rai hiyo amenitoa wakati akifungua ibada ya kusifu na kuabudu iliyoanda kwaya paradise ushirika wa Ruanda inayojulikana kama the Joy of praise lililofanyika katika ukumbi wa Tughimbe jijini Mbeya.‎‎

Kwaya ya paradise Moravian Ruanda Mbeya wakimtukuza Mungu kwenye tamasha lao(picha na Hobokela Lwinga)

Aidha Askofu Pangani amewataka vijana hao kuitumia ibada hiyo kwa ajili ya kujitafakari katika kuijiimarisha kiuchumi hali itakayowaondolea utegemezi ndani ya ushirika.‎‎

Mgeni rasmi katik ibada ni mtumishi wa Mungu Ikupa Mwaifwani ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya Ikupa financial services.

Baadhi wa washiriki katika ibada ya the Joy of Praise

‎‎Ibada hiyo imepambwa na kwaya mbalimbali ikiwemo Eden, Tumaini (maarufu kama shangilieni)kutoka arusha,Efatha Uhuru Moravian kutoka Dar es salaam.