Baraka FM
Baraka FM
25 June 2025, 12:08

Elimu haina mwisho kauli hiyo inathibitisha kuwa elimu haichagui umri wa mtu,bali elimu ni msingi wa maendeleo kwa mtu na taifa.
Na Hobokela Lwinga
Kaimu Katibu Mkuu kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi mch.Nsevilwe Msyaliha Ameitaka Jamii hasa vijana kuwa na maamuzi sahihi ambayo yatakuwa na mstakabali wa maisha yao ya maendeleo ya sasa na ya badae huku wakimtegemea Mungu.
Mch.Msyaliha ameyasema hayo wakati akifungua semina ya wazazi na walezi wa watoto yenye lengo la kutoa Elimu ya maambukizi ya virusi vya Ukimwi iliyofanyika katika kituo cha kulea watoto yatima kilichopo ndani ya chuo cha Moravian Chunya mkoani Mbeya kinachomilikiwa na kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi, Semina iliyoandaliwa na idara ya udiakonia na kufadhiliwa na shirika la mission 21.
Katika hatua nyingine Mch.Msyaliha amewataka washiriki Katika Semina hiyo kuzingatia yale yanayofundishwa na wakufunzi kwani yanafaida zaidi kwenye malezi.

Akifundisha ugonjwa wa UKIMWI katika Semina hiyo afisa mradi kutoka udiakonia Emmanuel Angetile amesema tafiti zinaonyesha kuwa maambukizi ya ukimwi nchini kwa watu ni elfu sitini kwa kila mwaka.

Kwa upande wake mkufunzi wa udiakonia katika semina hiyo Lulu Mpenja amesema kuna umuhimu mkubwa wa kuwasaidia watu wenye uhitaji kwani kufanya hivyo ni kumwakilisha Mungu katika utendaji wake duniani.

Baadhi ya washiriki katika Semina hiyo wamelishukru Kanisa huku wakisema elimu waliyoipata itawasaidia wao na watu wanaowazunguka.

Aidha katika semina hii watoto na wazazi wamepewa zawadi mbalimbali ikiwemo sukari, mafuta ya kupakaa,vifaaa vya shule Pamoja na bima za afya ambavyo vimetolewa na msimamizi wa vituo vya kulea yatima vya kanisa la Moravian Mch.Elizabeth Nampasa.

Huu ni mwendelezo wa seminar za udiakonia zinazoendelea kutolewa kwa watumishi wa kanisa la Moravian pamoja na vyuo vyake ,idara zake ikiwemo za kulea watoto yatima.