Baraka FM
Baraka FM
16 June 2025, 19:00

Thamani ya mtu iko mikononi vivyo hivyo thamani ya taasisi iko mikononi mwa mtu pia.
Na Hobokela Lwinga
Katika kuthamini mchango wa uandaaji wa maudhui ya kupigania haki za watu wenye ulemavu Shirika la Tanzania Joy Women Entrepreneurship for the Deaf (FUWAVITA) lenye makao makuu yake Jijini Dar es salaam limekitunuku kituo cha redio Baraka fm radio kinachomilikiwa na kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi.
Cheti hicho kimetolewa wakati wa kufunga mafunzo ya ujasiriamali kwa watu wenye ulemavu yaliyofanyika katika ukumbi wa kanisa la Moravian ushirika wa Rujewa wilayani Mbarali mkoani Mbeya.
Katika wa cheti hicho yameongozwa na Baba askofu Robert Pangani wa KMT -JKM akiongozana na mwandishi na Mtangazaji wa Redio Baraka @Hobokelalwinga.
