Baraka FM
Baraka FM
12 June 2025, 18:32

Kuelekea uchaguzi mkuu mwaka 2025 chama cha mapinduzi mkoa wa Mbeya waweka utaratibu wazi wa zoezi la uchukiaji wa fomu kwa ngazi za ubunge na udiwani.
Na Ezra Mwilwa
Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mbeya kimetoa utaratibu kuelekea wa mchakato wa uchaguzi wa Madiwani na Wabunge.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Katibu wa siasa na uenezi na Mafunzo Mkoa wa Mbeya Christopher Uhagile amesema Wajumbe wanne wa kamati ya siasa ya Mkoa wa Mbeya waneachia nafasi zao kwa kuwa wameoneaha nia ya kugombea nafasi mbalimbali.
Amesema mchakato wa utoaji fomu kwa nafasi ya udiwani na ubunge utaanza Juni 28,2025 pia ameonya wanachama watakaojaribu kuvuruga uchaguzi
Uchaguzi wa Madiwani, Wabunge na Rais utafanyika mwezi oktoba huku Chama Cha Mapinduzi kikidai kukamilika kwa maandalizi na ilani yake ya 2025/2030.