Baraka FM
Baraka FM
11 June 2025, 16:35

Jinamizi la ajali laendelea kuliandama jiji la Mbeya.
Na Hobokela Lwinga
Abiria waliokuwa wakisafiri kuelekea Tunduma kwa kutumia gari aina ya Coaster lenye namba za usajili T. 592 DKX linalofanya safari zake Mbeya – Tunduma wamenusurika kifo baada ya gari hilo kupata ajali eneo la Simike, jijini Mbeya.
Ajali hiyo imetokea mchana huu ambapo kwa mujibu wa abiria walionusurika katika ajali hiyo wamedai chanzo ni uzembe wa dereva kwa kutokuwa makini na barabara kwani hakukuwa na kikwazo chochote kilichopelekea kujikuta wapo mtaroni.
Itakumbukwa June 7,2025 Watu 28 walifariki dunia na wengine wanane kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha magari matatu ikiwamo lori na coaster katika mlima Iwambi jijini Mbeya.