Baraka FM

Watu 28 wafariki dunia ajalini Mbeya, Rais atoa mkono wa pole

8 June 2025, 14:22

Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya, Benjamin Kuzaga(Hobokela Lwinga)

Maisha ni hadithi na huwa yananyauka na kama maua,hali hiyo unaweza kuifananisha na maisha ya mwanadamu kwani huwa na nyakati tofauti mpaka kukifikia kifo.

‎‎Hobokela Lwinga ‎‎

WatuWatu 28 wamefariki dunia na wengine wanane kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha magari matatu ikiwamo lori na coaster katika mlima Iwambi jijini Mbeya.‎‎

Akithibitisha uwepo wa ajali hiyo Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya, Benjamin Kuzaga amesema ajali hiyo imetokea Jumamosi, Juni 7,2025 ambapo watu 27 walifariki papo hapo na majeruhi kuwahishwa Hospitali teule Ifisi iliyopo Mbalizi.‎‎

Sauti ya Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya, Benjamin Kuzaga

Kamanda huyo Amesema katika barabara kuu ya Tanzam kutokea Mbeya kwenda Tunduma, gari aina ya lori likiwa na tela likiendeshwa na dereva Philip Mwashibanda (33) liligonga magari mengine mawili.‎‎

Amesema katika magari hayo yaliyokuwa na abiria yaligongwa na lori hilo, kisha kutumbukia kwenye korongo ulipo Mto Mbalizi na kusababisha vifo na majeruhi hao.‎‎

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Mbeya Dkt.Juma homera ametoa salamu za pole na kuwaagiza TANROADS mkoa wa Mbeya kuanzia leo kutengeneza barabara ya mchepuo iliyopo eneo la iwambi.

Sauti ya Mkuu wa mkoa wa Mbeya akitoa maagizo kwa TANRODS
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Dkt.Juma homera akizungumza na wanahabari eneo la tukio (Hobokela Lwinga)

‎‎Dkt.Homera pia amesema Rais Samia ametoa pole kwa wafiwa wote kwa kugharamia majeneza ya Marehemu wote pamoja na mkono wa pole kwa kila familia kwa kuipatia shilingi 500,000.‎

Sauti ya akitoa salamu za Rais