Baraka FM
Baraka FM
29 May 2025, 17:31

Kanisa la Moravian linaoutaratibu wa watumishi wake kustaafu pale wanapofikisha umri wa miaka 60,umri huo unaendana na umri wa kustaafu kwa watumishi wa serikali.
Na Hobokela Lwinga
Waumini wa Kanisa la Moraviani Jimbo la Kusini Magharibi wametakiwa kujiandaa na kushiriki ibada maalumu ya kumuaga Makamu Mwenyekiti wa kanisa hilo itakayofanyika June Mosi mwaka huu katika ushirika wa Bethelehemu jijini Mbeya.
Wito huo umetolewa na Kaimu Katibu Mkuu wa Kanisa hilo Jimbo la Kusini Magharibi Mch. Nsevilwe Msyaliha wakati akizungumza na kituo hiki mapema leo.

Mch. Msyaliha amesema ibada hiyo itakuwa njema na yenye baraka kwa kila mmoja na kwamba itahudhuriwa na wageni kutoka madhehebu mbalimbali ndani na nje ya nchi.
Aidha amewataka Wachungaji wote kuvaa vazi la kichungaji siku hiyo muhimu iliyoandaliwa kwa ajili ya kumuaga Mchungaji Mwahalende kutokana na kazi kubwa aliyoifanya ndani ya kanisa na kuacha alama muhimu.