Baraka FM

Vishoka zao la pareto kukumbana na rungu la sheria

26 May 2025, 13:16

baadhi ya wakulima wa zao la pareto wakiwa na afisa pareto wa kampuni ya PCT mkoa wa Mbeya na Songwe Musa Malubalo(picha na Hobokela Lwinga)

Changamoto ya zao la pareto ni uwepo wa wanunuzi holela(vishoka) wasiofuata taratibu za ununuzi wa zao hilo.

Na Hobokela Lwinga

Serikali ya halmashauri ya wilaya mbeya imaahidi kuwashughulina kuwakamata wanunuzi walanguzi wanaowanyonya wakulima wanaojihusisha na kilimo cha pareto.

Akizungumza na wakulima wa zao la pareto wakati wa kupokea msaada wa dawati,blanket na vifaa vya shule vilivyotolewa na PCT kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya mbeya,afisa tarafa ya isangati Aron Sote amesema wananyonywa pasipo wao kujua.

Sote Amesema wakati zoezi hilo linaendelea wakulima hao wanapaswa kutoa ushirikiano ili kuwabaini wanunuzi wanunua zao hilo nje na utaratibu.

Sauti ya afisa tarafa ya isangati Aron Sote

Mmoja ya mawakala wa kampuni ya PCT Noel Adson Mwasile amesema mizani ambazo wao wanatumia kupimia pareto zimekaguliwa na wakala wa vipimo amewataka wwakulima kuuza kampuni ya pct ili waweze kupata tija.

Afisa pareto kampuni ya ununuzi wa pareto mkoa wa Mbeya na Songwe Musa Malubalo(picha na Hobokela Lwinga)
Sauti ya mmoja ya mawakala wa kampuni ya PCT Noel Adson Mwasile

Baadhi ya wakulima wamesema kukosekana kwa elimu ya uuzaji ndio sababu ya kuuza pareto kwa hasara huku wakiiomba serikali kuwashughulikiwa walanguzi wote kwa haraka ili kuondoa changamoto hiyo.

Sauti za baadhi ya wakulima wa zao la pareto Mbeya DC

kampuni ya PCT imakuwa ikiwatembelea wakulima kwa lengo la kujua na kutambua changamoto mbalimbali zinazowakabili wakulima.